MAHAKAMA MKOANI SINGIDA YA TEKETEZA KILO 359 ZA BANGI
Posted on
Jul 9, 2012
|
No Comments
Askari Polisi, Sebastian Tall akiteketeza bangi kilo 350 kwa amri ya mahakama.
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoani Singida, imeteketeza kilo 350 za bangi aliyokamatwa nayo Pascal Bangii(31), Wilaya Nzega Mkoani Tabora, na kukiri kosa lake kabla ya kuhukumiwa miaka kumi jela.
Uharibifu huo umefanywa kwenye viwanja vya Mahakama chini ya hakimu Chiganga Tengwa, Flora Ndale na ulinzi mkali wa jeshi la Polisi, Mjini Singida, huku ukishuhudiwa na baadhi ya Wananchi.
Kijana Bangii alikamatwa na Polisi Juni 29, 2012, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema, wakati akisafirisha bangi hiyo yenye thamani ya Sh. 5,250,000, kwenda Dar es Salaam, kwa kutumia usafiri wa basi.
Aliyetoa hukumu hiyo ya kifungo cha miaka kumi jela ni hakimu Chiganga Tengwa, na alifanya hivyo baada ya mshitakiwa huyo kukiri mara tatu na hivyo kupigwa faini ya Sh. Milioni 15 au kifungo cha miaka kumi gerezani.