photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WEMA SEPETU ALIKAMATA JICHO LA RAIS WA BURUNDI

WEMA SEPETU ALIKAMATA JICHO LA RAIS WA BURUNDI

Posted on Jul 9, 2012 | No Comments

Umaarufu wa Miss Tanzania (2006) Wema Sepetu ambaye juzi alichezea kichapo kutoka kwa Jackline Wolper kwenye pambano la ndondi, umeendelea kuvuka border na sasa rais wa Burundi anataka aendee Ikulu.
Gazeti la Ijumaa Wikienda limesema kuwa mrembo na muigizaji huyo amealikwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.
Ameliambia gazeti hilo kuwa mwaliko huo aliupata siku chache baada ya kuzindua filamu yake ya Super Star jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amemwalika pia muigizaji wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade.
Ujumbe kutoka ikulu ya Burundi umemtaka Wema kutoisambaza kwanza filamu hiyo nchini humo kabla ya kuizundua (ofcourse ili kupiga hela zaidi)
 “Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema.
Dalili zinaoenesha kuwa filamu yake ya Superstar itafanya vizuri sokoni.

Tunamtakia kila lakheri.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru