MGOMO WA MABASI WASABABISHA TABU KWA WASAFIRI ARUSHA NA MOSHI.
Posted on
Jul 10, 2012
|
No Comments
Vuta nikuvute kati ya uongozi wa Manispa ya Moshi, madereva na viongozi wa chama cha usafirishaji kanda ya Kaskazini (Akiboa), ya kupinga ongezeko la ushuru katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi, imeingia siku ya tatu huku wananchi wakiendelea kutaabika.
Kwa siku ya jana kumekuwa na mgomo usio na kikomo ambapo tangu asubuhi daladala zote zinazotoa huduma ya usafiri mjini hapa, nje ya mji kwa maana ya wilayani na kwenda mkoani Arusha, ziligoma na kuondoa magari katika kituo cha mabasi.
Madereva na wamiliki wa magari yanayofanya safari zake mkoani Kilimanjaro na Arusha, kugoma kufanya kazi kwa kile wanachodai kuwa ni kutoshirikishwa katika mchakato wa kupandishwa kwa ushuru kutoka Sh. 1,000 hadi 1,500 kwa magari madogo na Sh. 2,000 kwa magari makubwa.
NIPASHE ilishuhudia abiria wakiwa wametanda maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi, husasani katika kituo kikuu cha mabasi huku wakiwa hawajui hatma yao, huku suala hilo likiwa ni neema kubwa kwa madereva teksi, Noah na pikipiki, ambao walibeba abiria kwa gharama kubwa.
Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa Akiboa, Husseini Mrindoko, alisema hawako tayari kulipa
ushuru huo na kuongeza kuwa watarudisha magari yao barabarani hadi ushuru utakaporudishwa Sh. 1,000 kama iliyo kuwa awali.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Christopher Mtamakaya, alisema utaratibu wa kupandishwa kwa ushuru ulifuata hatua zote za kisheria na kwamba kabla ya kupitishwa wadau wote walishirikishwa hatimaye kufikia kusainiwa na Waziri Mkuu kwa ajili ya utekelezaji.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Ibrahim Msengi, akitoa msimamo wa serikali kuhusu mgomo huo alisema, serikali inatambua adha wanayoipata wananchi na kuwataka wawe wavumilivu wakati ikilitafutia ufumbuzi.
Kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya vyama vya siasa kujiingiza katika sakata hilo na kuchochea mgomo huo.
Baadhi ya abiria waliongea na NIPASHE, Neema Msuya na Elisamehe Juma, walisema mgomo huo umewaathiri kwa kiasi kikubwa kwani wemeshindwa kufika kazini kwa wakati.
“Nimetoka nyumbani nakwenda hospitali ya rufaa ya KCMC kuangalia mgonjwa, nimekwama hadi saa 1:30 asubuhi sijapata usafiri…tunaiomba serikali kuingilia kati kutatua suala hili, watu waache ushabiki ambao mwisho wa siku wanaoumia ni wananchi, nimetumia shilingi 4,000 kwenda na kurudi KCMC,” alisema Abel Anthony.
Mkoani Arusha abiria walionja adha ya mgomo huo baada ya kukwama kwa wale waliokuwa wakitoka mjini hapa kwenda Moshi hasa nyakati za jioni jana.
Majira ya asubuhi mamia ya abiria walipanda mabasi makubwa yanayofanya safari zake kutoka mjini Arusha hadi mikaoni mingine kama ya Tanga, Dar es Salaam na Morogoro.
Kwa kawaida mabasi mengi yanayoenda mikoa hiyo huanza safari zake alfajiri hadi majira ya saa 5 asubuhi, hali ambayo inawawezesha abiria wanaoshuka mjini Moshi kupanda mabasi hayo.
Ugumu wa usafiri ulionekana zaidi jioni, baada ya abiria kutoka sehemu mbalimbali mkoani hapa na wengine kutoka Babati kukosa usafiri wa kwenda mjini Moshi.