photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC LAPATA VIONGOZI WAPYA

TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC LAPATA VIONGOZI WAPYA

Posted on Jul 16, 2012 | No Comments

 Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.
 Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.
 Kutoka kushoto Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.
Mzee Emmanuel Muganda pamoja na Mkewe wakiwapa mawili matatu Uongozi mpya wa  Chadema Washington DC.Picha na habari na Mdau Swahili Villa

Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokwa Viongozi wa muda.

Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi.

Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyevitina Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.

Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia Katibu mya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru