photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TASWIRA MBALIMBALI JINSI VIONGOZI WA CCM NA SERIKALI WALIVYOUNGURUMA KATAVI

TASWIRA MBALIMBALI JINSI VIONGOZI WA CCM NA SERIKALI WALIVYOUNGURUMA KATAVI

Posted on Jul 16, 2012 | No Comments

Naibu Waziri TAMISEMI,Mh.Aggrey Mwanri akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi,ambapo aliwasihi kutokubali kudanganywa danganywa na pia aliwaambia wananchi serikali hii isingependa kuona wananchi wa chini akionewa, hivyo alitoa tamko la kutowalipisha ushuru wakina mama wafanya biashara ndogo ndogo mfano vitumbua na chapati.
Naibu Waziri Kilimo na chakula,Mh. Adam  Malima akihutubia wananchi wa mkoa wa Katavi, juu ya masuala mabali mbali ambayo yametekelezeka likiwemo suala la umeme na pia aliwaambia wakulima kwamba serikali imeandaa utaratibu mzuri wa vocha za kilimo ambazo utatangazwa hivi karibuni.
Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba akizungumzia masuala ya kuimarisha reli na pia  utunzaji wa treni zetu ikiwa suala zima la usafi, pia aliwaambia wananchi serikali imeagiza mabehewa ya abiria na ya mizigo.
Mh.Nape akihutubia wananchi wa Mpanda waliofurika kwenye  uwanja wa Kashaulili,ambapo alikemea vikali vitendo vya vyama vingine kuendekeza vurugu badala ya siasa.
Mh.Mwigulu Mchemba akieleza wananchi masuala muhimu ya kiuchumi na kwa nini kunakuwa na mfumuko wa bei,pia alitumia fursa hiyo kukemea mauaji yalotokea kwenye jimbo lake ambapo kijana mmoja kiongozi wa chama aliuawa na wanachama wa chama cha upinzani
  Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa-Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru