photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> MAKALA; TUWAHURUMIE WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

MAKALA; TUWAHURUMIE WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Posted on Jul 14, 2012 | 2 Comments

Tatizo la watoto wa mitaani linalo julikana na jamii nzima la kujiuliza ni je,Watoto hao wanapata msaada gani ?
Watoto hao wamekuwa wakilalamikia serikali na jamii kila kukucha lakini malalamiko yao yamekuwa yakipuuzwa ou kutokuchukuliwa hatua zozote
Ipo kauli pia  wanapelekwa  kwenye vituo vya watoto yatima na kuachwa bila msaada wowote hilo husababishwa na maisha kuwa magumu kwao.
Wamekuwa  wakichukuliwa  na kupelekwa katika vituo vya kulelea watoto yatima,lakini mwisho wake wanaishia kutoroka kutokana na mazingira kuwa magumu wanayo kumbana nayo.
Kulingana na maelezo yao wamekuwa wakidai kuwa maisha ya vituo vya kulelea watoto yatima yamekuwa ni magumu bora ya mitaani.Ninaloliona ni serikali na jamii kwa ujumla  kuwapa kipaumbele watoto wa mitaani.
Watoto hao ambao wamekua wakilalamikia serikali kutokufanya mkakati wa kuwasaidia hadi ifikapo kipindi cha uchaguzi au katika kipindi ambacho jamii inaitaji kitu Fulani na ndiyo nayo inakumbukwa.
Maisha bila msaada wowote ni magumu mno,kama jinsi inavyo julikana na watanzania wengi wenye kiwango cha chini cha kujikimu kimaisha.
Baada ya kuongea na baadhi ya watoto wa mitaani na kusikiliza hoja zao naomba serikali na jamii kuweka mikakati madhubuti kuhusiana na sualala uangalizi la uangalizi wa watoto wa mitaani,yatima na wasio jiweza  kwani kwa kufanya hivyo itakuwa hatua kubwa ya kupunguza wizi,ujambazi na matatizo ya mmonyonyoko wa maadili kwa jamii yetu.
Serikali imejaribu kuchukua hatua tofauti katika kuakikisha watoto hawa wa mitaani wanapata haki na malezi mazuri.Mikakati ya kuakikisha watoto hawa wanapata elimu sawa na wengine anatakiwa iwepo ingawa nayo inaitaji nayo inaitaji umakini katika uchanganuzi wa nani naitaji zaidi ya mwingine.
Jamii ina jukumu la kuwalinda na kutetea haki za watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu kwani wana haki zote za kulindwa na kupatiwa msaada ipasavyo.kuwasaidia watoto hawa ni sawa na kuwapelekea maendeleo katika jamii husika.
Kuwapeleka watoto hao katika vituo vya kulelea  yatima si kukamilisha au kutatua  matatizo yanayo wakabili,bali penginepo ni kuwaongezea majukumu.
Kutokana na malalamiko yao ni kwamba katika vituo hivyo inakuwa ngumu kwa wao kijikimu kimaisha bila msaada wowote kutoka kwa jamii au serikali.
Hivyo kupelekea kwa wao kuona ni maisha magumu na wengineo kuamua kutoraka katika vitu hivyo.
Kutokana na mateso hayo wanayoyapata watoto hao wanaamua kujiingiza katika uovu,ikiwemo wizi na ubakaji,kuangalia ukuwaji wa watoto hawa ni jukumu la serikali na jamii yote kwa ujumla kwani inamhusu kila mtu.
Wengi hawana sehemu ya kulala ifikapo usiku hivyo hulala kwenye mitaro ,kwa watoto hao kupelekwa katika vituo vya kulelea watoto yatima na makazi na uwezo wa kujikimu sio kumaliza tatizo lao. Kwani mara nyingi kutokea maisha kuwa magumu katika katika vituo kuliko mitaani.
Mtaani wanakuwa na uwezo wa kuangalia kufanya biashara ndogondogo  ili kuweza kutatua tatizo la ugumu wa maisha.inawawia vigumu sio kwao bali kwa mtu yoyote,kukaa na njaa na kutokujua leo wala kesho utakula nini na utapata wapi chakula hicho.
Ni wito kwetu kuangalia watoto hawa wanaishi vipi na ni jambo gani linaweza kufanyika ili kuakikisha kuwa vijana hawa wanakuwa na maisha kuweza kujikimu na waweze kupata haki zao za kimsingi ikiwemo elimu.
Jamii inatakiwa kufanya kitu ili tatizo hili lisiendelee kuumiza kundi hili kubwa ambalo ni tegemezi kwa taifa hili kesho.
Msaada kwa vijana hao si wa kifedha tu bali hata mavazi na malezi na wapo wengine wao ambao shida yao kuu ni kupata nauli ya kurudi mikoani kwao tu.
Serikali kama chombo kikuu cha utegemezi kwa wananchi  kimekuwa kikijitolea kwa mambo mengi kwa dhumuni la kuwasaidia vijanahawa lakini imekuwa haijitoshelezi,ivyo basi msaada zaidi unaitajika kwa lengo la kutatua tatizo hili.
                                
Na mwandishi wetu  
PETER .L.UISO 
0713-162905


Comments: 2

  1. KAKA KUNA EDITING ERRO PALE JUU SAMAHANI KM UNAWEZA KUREKEBISHA NISAIDIE

    ReplyDelete
  2. Small companies will use pledging or factoring
    accounts receivable to boost money payday loans unsecured unemployed loans are
    a fairly easy and manageable way to get supplemental income.
    My site: payday loans

    ReplyDelete