photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MATUKIO YA MISS SINZA 2012 KATIKA PICHA..

MATUKIO YA MISS SINZA 2012 KATIKA PICHA..

Posted on Jul 14, 2012 | No Comments


Miss Sinza 2012, Brigitte Alfred, akiwa mwenye tabasamu kali la furaha baada ya kufanikiwa kuvikwa taji la Miss Sinza 2012 katika Shindano la Miss Sinza 2012 lilifanyika usiku wa kuamkia Juni 13,2012 katika Ukumbi wa Mawela Sinza Jijini Dar es Salaam. Brigitte mrembo aliyekuwa chaguo la wengi ukumbini hapo licha ya kuchuana vikali na mshindi wa pili na watatu aliwashinda warembo wengine 13 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja nae.
Miss Sinza 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu Esther Mussa. Shindano la Miss Sinza 2012 lilifanyika usiku wa kuamkia Juni 13,2012 katika Ukumbi wa Mawela Sinza Jijini Dar es Salaam.
 
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012 wakipozi kwa picha jukwaani.
 Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Vivian Sirikwa akitangaza washindi
 
  Warembo wakipita jukwaani na kupozi kwa picha wakati wa kujinadi mbele ya majaji kwa kivazi cha ufukweni.
 
 ...na kundi zima la African Stars au Twanga Pepeta
 Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Prashant Patel (kushoto) na Katibu Wake Bosco Majaliwa 'Mshua' na mrembo wa Miss Tanzania 2011, Hamisa wakifuatilia shindano hilo.
Jopo la Majaji likifuatilia kwa umakini shindani hilo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru