photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > UCHAGUZI NAIBU MEYA ARUSHA WAAHIRISHWA

UCHAGUZI NAIBU MEYA ARUSHA WAAHIRISHWA

Posted on Jul 10, 2012 | No Comments

KATIKA hali isiyo ya kawaida ule uchaguzi wa Naibu Meya uliotarajiwa kufanyika  jana ndani ya ukumbi wa Halmshauri ya Manispaa ya Arusha umeahirishwa ghafla kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya madiwani wa Chadema jijini hapa kuupinga kwa madai kwamba umekiuka taratibu,sheria na kanuni za kudumu za halmashauri hiyo.

Hata hivyo,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Estomi Chang”a alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi huo huku akisisitiza kuwa ni kutokana na kubanwa na majukumu mengine ya mkoa na wilaya  ambayo hakuyafafanua kwa kina.

Juzi gazeti hili lilifichua habari za uchaguzi wa naibu meya kufanyika jana ndani ya manispaa hiyo ambapo  madiwani wa manispaa hiyo waliandikiwa barua za wito na ratiba nzima ya uchaguzi huo wa kujaza nafasi ya unaibu meya wa jiji la Arusha.

Habari zilizopatikana leo zimedai ya kwamba muda mchache tu baada ya madiwani wa Chadema kupokea barua za uchaguzi huo walipinga kwa nguvu zote kwa  kumwandikia mkurugenzi wa manispaa hiyo barua nzito ya kuupinga uchaguzi huo.

Taarifa zimedai  kwamba Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Isaya Doita ambaye pia ni diwani wa kata ya Ngarenaro alimwandikia mkurugenzi huyo barua hiyo huku akisema kwamba wanapinga uchaguzi huo kwa kuwa umekiuka kanuni na taratibu za kudumu za halmashauri hiyo.

Katika barua hiyo  diwani huyo alimwandikia mkurugenzi sababu za kuupinga  kwamba walichelewa kupewa taarifa za uchaguzi huo na vyama husika vilipaswa kupewa taarifa mapema ili viweze kujiandaa kwa kuwa vyenyewe ndivyo vyenye dhamana ya kuteua wagombea.

Hata hivyo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha alipoulizwa na gazeti hili kuhusu taarifa za uchaguzi huo alikiri uongozi wake kupanga ufanyike jana,  lakini alisisitiza kwamba wameuahirisha kutokana na kubanwa na majukumu ya mkoa na wilaya ambayo hakuyafafanua.

Chang”a, alisema  ratiba ya uchaguzi huo ulipaswa kuanza jana ambapo vikao vya vyama vilipaswa kukaa kwa kufuatiwa na baraza la uchaguzi wa kujaza nafasi ya naibu meya na wenyeviti wa kamati za kudumu kulingana na kanuni kwa kuwa muda wao umemalizika.

“Ndiyo jana vilikuwa vifanyike  vikao vya vyama na  leo baraza la uchaguzi wa naibu meya na wenyeviti wa kamati za kudumu kulingana na kanuni muda wao wa mwaka umekwisha,hata hivyo tumeahirisha kutokana na kubanwa na majukumu mengine ya mkoa na wilaya”alisema mkurugenzi huyo.

Naye,Doita  alipoulizwa kuhusu hatua yake ya kuupinga uchaguzi huo alikiri taarifa za kuupinga kwa madai kwamba umekiuka taratibu,sheria na kanuni za kudumu za halmashauri hiyo  kwa kuwa vyama husika havikupewa taarifa  na hata wao hawakujulishwa mapema.

Alipoulizwa ya kwamba endapo taratibu hizo zikifuatwa je wako tayari kwenda kwenye uchaguzi?,  alijibu kuwa wanasubiri maamuzi ya kamati kuu ya Chadema ambayo inafanya vikao vyake jijini Dar es salaam hivyo asingependa kulijibu swali hilo.

Uchaguzi wa Naibu Meya jijini Arusha ulizua mtafaruku mwaka juzi baada ya Diwani wa Kata ya Sokon One,Michael Kivuyo kupitia TLP kujiuzulu nafasi hiyo na kuacha kiti hicho wazi, hata hivyo mwaka jana baadhi ya madiwani wa Chadema na CCM waliingia muafaka wa kutatua mgogoro wa umeya wa Arusha ambapo walimchagua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimandolu,Estomi Mallah kitendo kilichopelekea kutimuliwa na kisha kuvuliwa unachama ndani ya Chadema.

Mallah,alitimuliwa ndani ya Chadema na kamati kuu ya chama hicho akiwa na madiwani wenzake wanne ambao ni pamoja na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Themi, Ruben Ngowi, .Diwani wa Kata  ya Kaloleni,Charles Mpanda”Rasta”,Diwani wa Kata ya Elerai,John Bayo sambamba  na diwani wa viti maalumu,Rehema Mohammed
 
Source; Mwanachi 

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru