ETHIOPIA YAWA YA KWANZA AFRIKA KUNUNUA NDEGE AINA NA ‘BOEING 787 DREAMLINER’.
Posted on
Aug 21, 2012
|
1 Comment
Shirika la Ndege la Ethiopia limekuwa la kwanza kumiliki ndege kubwa na ya kisasa kwa nchi za Afrika aina ya ‘Boeing 787 Dreamliner, na kuifanya kuwa nchi pekee Afrika kutumia ndege ya aina hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Ethiopian Airliner Tewolde Gebremariam amesema kwa kufikia uwezo huo inaonyesha jinsi gani Afrika inavyopiga hatua katika maendeleo duniani.
Ndege hiyo imewasili nchini Ethiopia kutoka uwanja wa ndege wa Dulles mjini Washngton, ambako kunaishi raia wengi wa Ethiopia.
Ndege hiyo mali ya Shirika la Ndege la Ethiopia linaloongoza kwa kukua kwa kasi, limenunua ndege hiyo kwa takriban dola milioni 207 za Marekani.
it deserves, since it was not colonised
ReplyDelete