photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > JE WAJUA JINSI WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

JE WAJUA JINSI WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Posted on Aug 21, 2012 | No Comments


Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa ya kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na yenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hiyo kama tiba
ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa wengi kati
ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati
yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa wanaimiliki daima.
Lakini, watafiti wa masuala
ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hiyo.
Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.


Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu za siri kwa sababu
ya kushindwa katika tendo. Hali hii inatoa picha kwamba mzigo wa lawama hujitwika wenyewe.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:


1: KAULI

Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litamfanya aanze kupoteza nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwabia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu kwa kuwaambia maneno kama ha
ya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI

Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume husika kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfan
ya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na u
elewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

USAFI

Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi ni muhimu sana katika mapenzi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru