photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MEGATRADE YAIMWAGIA VIFAA TIMU YA POLISI KILIMANJARO

MEGATRADE YAIMWAGIA VIFAA TIMU YA POLISI KILIMANJARO

Posted on Aug 15, 2012 | No Comments

 Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd Goodluck Kway akimkabidhi kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert 
Baadhi ya vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya Polisi Kilimanjaro.
 
KAMPUNI ya Megatrade Investiment Ltd kupitia kinywaji chake cha K-Vant Gin imeamua kuidhamini timu ya mpira wa miguu ya Polisi Kilimanjaro ili kufanikisha ushiriki wake katika ligi ya mpira wa miguu ya Polisi jamii mkoa wa Kilimanjaro
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu hiyo,meneja mauzo na masoko wa kampuni hiyo Goodluck Kway amesema hatua hiyo ni mipango ya Megatrade kurudisha faida kidogo inayopata  kwa jamii kupitia njia ya michezo.
Amesema kwa kuthamini michezo ,mchango wa jeshi la polisi katika ulinzi na usalama wa raia pamoja na dhana nzima ya ulinzi shirikishi au polisi jamii kampuni hiyo imeamua kudhamini timu hiyo ili kuongeza hamasa katika mahusiano baina ya askari polisi na raia.
Kway alisema vifaa vilivyotolewa vinathamani ya kiasi cha shilingi milioni 6 ambavyo ni seti moja ya jezi,viatu jozi 18,glovu za mlinda mlango seti mbili,mipira 4,vizuia ugoko seti 18 na suti za michezo.
"Ni matumaini yetu kuwa vifaa hivi vitaongeza hamasa katika ushiriki wenu katika michezo hii na pia mtakuwa mabalozi wazuri wa kinywaji cha K-Vant"alisema Kway.
Kwa upande wake kamanda Boaz ameishkuru kampuni ya Megatrade kwa msaada huo na kwamaba umekuja wakati muafaka wakati jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro likijiandaa kuirejesha timu  yake katika medani ya soka baada ya kupotea kwa takribani miaka 5

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru