PRINCE PHILIP ALAZWA HOSPITALINI
Posted on
Aug 15, 2012
|
No Comments
Prince Philip |
Mume wa Malkia wa Uingereza, ambaye rasmi ni ''Duke wa Edinburgh'' amelazwa hospitalini kwa kile kilichotajwa kama hatua za tahadhari kufuatia maradhi ya kibofu yanayomsumbua, ka mujibu wa tangazo la Kasri ya Malkia ya Buckingham.
Prince Philip, ambaye ana umri wa miaka 91, alisafirishwa kwa gari la wagonjwa na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi huko Aberdeen ambako huishi pamoja na Malkia.
Prince Philp aliwahi kukumbwa na maradhi haya siku chache kabla ya sherehe za miaka 60 tarehe 6 Juni.
Anatazamiwa kukaa huko kwa siku kadhaa zijazo. Mwana wa mfalme Charles na mkewe 'Duchess wa Cornwall'' wako katika makaazi yao yasiyo rasmi ya Birkhall kwenye Makaazi ya Balmoral huku Mwana wa mfalme William na mkewe wameungana na Malkia huko Balmoral.
Haijafahamika kama wana wa nyumba ya Kifalme wamekwenda kujiunga na Malkia au la.