photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SIMBA NA CHUI KATIKA MAONESHO YA NANENANE MWAKA HUU

SIMBA NA CHUI KATIKA MAONESHO YA NANENANE MWAKA HUU

Posted on Aug 7, 2012 | No Comments



CHAMA  cha Wakulima na Wafugaji kwa kanda ya kaskazini(TASO) kimesema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa na mabadiliko makubwa hasa kwa upande wa Ufugaji ambapo ndani ya maonesho hayo pia kutakuwa na maonesho ya wanyama mbalimbali kama vile Simba na Chui huku lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha zaidi kilimo kwanza hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw Athur Kitonga wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini hapa kuhusiana na maonesho ya wakulima na wafugaji kwa mwaka huu (Nane nane).

Bw Kitonga alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa ni maonesho ya tofauti na miaka mingine kwa kuwa kwa sasa wamewapa vipaumbele zaidi wafugaji na wakulima katika maonesho hayo tofaiuti na Miaka mingine ambayo kuna kuwa na wafanyabiashara wengi zaidi kuliko waoneshaji

Pia alisema kuwa ndani ya maonesho hayo ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza rasmi kuanzia kesho mpaka Agust 10 mwaka huu  kutakuwa na wanayama mbalimbali kama Vile Simba na Chui kutoka Jijini Dar es saalam ambapo napo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa ufugaji unakuwa ni wa kisasa zaidi

“tunatarajia kuleta Simba na Chui katika maonesho haya ya Nane nane huku lengo letu nin kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajua kuwa wanyama kama hawa wanaweza kuwa marafiki  wa binadamu na kwa hali hiyo ufugaji utaimarika sana kwa kuwa wanannchi nao watapata elimu zaidi kuhusiana na wanyama kama hawa”aliongeza bw Kitonga

Akiongelea idadi kubwa ya wafanyabaishara kuliko wakulima na wafugaji alisema kuwa lengo halisi la Maonesho hayo ni kuhakikisha kuwa walengwa wanapata haki zao za msingi na wala sio biashara ndogondogo na kwa hali hiyo asilimia kubwa watakuwa ni wafugaji na wakulima

“katika maonesho mengine kama mnavyojua idadi kubwa sana wanakuwa ni machinga wakati chama hiki kwa sasa kina malengo ya kumboresha mkulima na mfugaji wa kanda hii ya kaskazini kwa maana hiyo basi ndani ya maonesho haya hatuitaji kuona Machinga wakiwepo bali wawepo wale ambao ni walengwa wa chama na Maonesho haya”aliongeza bw Kitonga

Pia alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa malengo ya Kilimo kwanza yanafikiwa tena kwa wakati Chama hicho kimejipnga kwa kuhakikisha kuwa washiriki wote ambao wanashiriki maonesho hasa kwa wale ambao wataonekana kutoa elimu zaidi kwa wakulima na wafugaji bora watapata zawadi  ambazo zinalenga kuendelea kuimarisha zaidi Kilimo kwanza hapa nchini.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru