WAFANYABIASHARA WA MADINI WAIOMBA SERIKALI KUANZISHIWA BENKI
Posted on
Aug 6, 2012
|
No Comments
WAFANYABISHARA wa madini mkoani Arusha wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuanzisha benki yamadini hapa nchini itakayo wasaidia kuuza madini yao na kuepusha utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi unaofanywa na baadhi yao wasio waaminifu kwa kutumia njia za panya.
Aidha wametaka kuanzishwa kwa chuo cha ukataji madini hapa nchini ,tofauti na sasa ambapo madini mengi yamekuwa yakisafirishwa na kukatwa nchini Kenya , hali ambayo imesababisha wafanyabiashara wakubwa duniani kuishia nchini humo na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato ya serikali.
Akizungumzia swala hilo mmoja wa wafanyabishara wa madini mjini hapa,Joel Saitoti alisema kuwa, ni vema serikali ikaangalia uwezekano wa kuanzisha benki ya madini hapa nchini,kwani itasaidia wao kuuza madini yao kwa uhakika zaidi .
Pia alisema kuanzishwa kwa benki hiyo itawabana wafanyabishara wa kigeni wa madini wanaoingia nchini na kukunua madini kinyume na utaratibu kwa kutumia wachuuzi tofauti na leseni zao zinavyoelekeza.
Alisema kuwa kwa sasa wanunuzi wa madini kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingia nchini na kununua madini yenye uzito hata usioruhusiwa kwa kutumia wachuuzi waliopo migodini,ambapo maelekezo ya leseni zao yanawataka kununua madini hayo kwa wafanyabiashara wakubwa .
Aidha alitumia fursa hiyo kuishauri seriakali kuanzisha chuo maalumu cha kufundisha jinsi ya kukata madini ambacho kitakuwa na wataalamu wenye uzoefu kutoka nchi za India, Tailand na China huku serikali ikiwapa wataaalamu hao kibali cha kuishi nchini wakati wakitoa elimu hiyo.Aidha wametaka kuanzishwa kwa chuo cha ukataji madini hapa nchini ,tofauti na sasa ambapo madini mengi yamekuwa yakisafirishwa na kukatwa nchini Kenya , hali ambayo imesababisha wafanyabiashara wakubwa duniani kuishia nchini humo na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato ya serikali.
Akizungumzia swala hilo mmoja wa wafanyabishara wa madini mjini hapa,Joel Saitoti alisema kuwa, ni vema serikali ikaangalia uwezekano wa kuanzisha benki ya madini hapa nchini,kwani itasaidia wao kuuza madini yao kwa uhakika zaidi .
Pia alisema kuanzishwa kwa benki hiyo itawabana wafanyabishara wa kigeni wa madini wanaoingia nchini na kukunua madini kinyume na utaratibu kwa kutumia wachuuzi tofauti na leseni zao zinavyoelekeza.
Alisema kuwa kwa sasa wanunuzi wa madini kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingia nchini na kununua madini yenye uzito hata usioruhusiwa kwa kutumia wachuuzi waliopo migodini,ambapo maelekezo ya leseni zao yanawataka kununua madini hayo kwa wafanyabiashara wakubwa .
Aliongeza kuwa, endapo chuo hicho kitaanzishwa hapa nchini kitasaidia sana kupata wataalamu wazuri ambao watajua kukata madini kitaifa ,ambao watakuwa wamejifunza jinsi ya kukata madini hayo na hatimaye kuweza kufanya shughuli hiyo kwa uhakika zaidi , lakini kwa sasa hivi madini yote yanatoroshewa nchini Kenya na wageni wengi wanaishia huko.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini nchini Tamida ,Jammy Mollel alisema kuwa iwapo Benki ya wafanyabiuashara wa madini itaanzishwa itawasaidia kupata mikopo ili waweze kununua vifaa mbalimbali vya
uchimbaji madini pamoja na kupata mikopo mbalimbali ya fedha kupitia benki hiyo.
Hata hivyo, aliiomba serikali kuwasaidia kuondoa kodi
ya VAT ya asilimia 18 ambayo inawafanya baadhi ya wafanyabiashara wa madini hayo kutumia njia za panya kwa ajili ya kusafirisha madini kwenda Nchini Kenya.
ya VAT ya asilimia 18 ambayo inawafanya baadhi ya wafanyabiashara wa madini hayo kutumia njia za panya kwa ajili ya kusafirisha madini kwenda Nchini Kenya.
'Jamani tunaomba sana serikali yetu itusikilize katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili katika kuhakikisha kuwa wanatuondolea kodi hii kwani imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa sana kuwepo kwa utoroshaji wa madini kwa njia za panya kutokana na wengi wao kukwepa kodi hiyo'alisema Mollel.
Aidha aliiiomba serikali pia kutowaruhusu wawekezaji wa kigeni kutoka nje ya nchi kutoingia ndani ya migodi kuyafuata madini hayo hali ambayo imekuwa ikichangia kuzorota kwa soko la madini na kuwasababishia wafanyabishara wakubwa kutopata wateja .
Aliongeza kuwa, wachimbaji wa kigeni wanapaswa kununua madini hayo kwa wafanyabiashar wakubwa na wanaotambulika na wenye leseni na sio kwende kufutana madini kwenye migodi kama wengine wanavyofanya na hao ndio wanachangia kufa kwa soko la madini hapa nchini.
Kwa upande wa kamishna wa madini kanda ya kaskazini,Benjamin Mchwampaka alisema kwa sasa serikali haiwezi kusema kitu kwa kuwa maombi ya wafanyabiashara hao bado hawajayafikisha rasimi serikani zaidi ya kuona kwenye vyombo vya habari.