photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TAARIFA YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM

TAARIFA YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM

Posted on Aug 26, 2012 | No Comments

 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es salaam tarehe 24/08/2012 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanya yafuatayo;-
 
#. Imepokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa maagizo yake juu ya kushughulikia mapungufu yaliyoonyeshwa kwenye taarifa ya CAG na Kamati mbalimbali za bunge.
#. Imeipongeza serikali kwa hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya mapungufu hayo, hasa hatua dhidi ya wakuu mbalimbali wa mashirika kadhaa ya umma, kama vile TANESCO, TBS,  BANDARI , ATC,MALIASILI nk.
**Itakumbukwa Kamati Kuu iliagiza pamoja na viongozi wa kisiasa kuchukuliwa hatua kwa mapungufu yale, ipo haja ya kuwachukulia hatua watendaji wakuu wa mashirika yaliyohusishwa na ubadhirifu mbalimbali. 
 #. Kamati Kuu inawapongeza mawaziri husika na watendaji wote wa serikali walioanza kutekeleza agizo hili kwani mwisho wa siku maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana.
 #.Pamoja na pongezi hizo, Kamati Kuu imeielekeza serikali kuendelea kuchukua hatua zaidi ili kufikia lengo lililokusudiwa.
 #. Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania kwenye ziwa Nyasa na hatua zilizochukuliwa kutatua mgogoro huo. Kamati kuu ikaazimia yafuatayo;
 (i). Imeipongeza serikali kwa hatua inazochukua za kupata suluhisho la mgogoro huo kwa njia ya amani.
(ii). Kamati Kuu inawatahadharisha wanasiasa na vyombo vya habari vinavyochochea vita na uhasama kati ya Tanzania na Malawi kuacha mara moja na kuiachia diplomasia ichukue mkondo wake.
(iii). Kamati Kuu imeitaka serikali kwakuwa tatizo hili limekuwa la muda na linajirudia mara kwa mara sasa kulishighulikia swala hili mpaka mwisho.
 #.  Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya maendeleo ya uchaguzi ndani ya Chama, iliridhishwa na maendeleo hayo ya uchaguzi na kuagiza yafuatayo;-
(i). Kila kikao husika kihakikishe haki inatendeka hasa katika zoezi la uchujaji wa majina.
(ii). Kuendelea kukemea vitendo vya rushwa kwenye chaguzi zetu. Na kuhakikisha kila anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo au mawakala wao hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
(iii). Kamati Kuu imeyapongeza mashina, matawi na kata zilizokamilisha zoezi hili kwa ufanisi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru