CHADEMA YAMTANGAZA MSAJILI WA VYAMA BW. JOHN TENDWA KUWA ADUI WA DEMOKRASIA.
Posted on
Sep 10, 2012
|
No Comments
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Siasa cha Upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Freeman Mbowe (Mb) (katikati) akitoa maazimio ya Kamati Kuu ya yaliyotolewa katika kikao maalum. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Wilbrod Slaa na kushoto ni Makamu Mwenyekiti Taifa Bw. Said Issa Mohammed.
Amesema moja ya ya maazimio ya Kamati Kuu ni kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, CHADEMA haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bw. John Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine.