photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > RAIS KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI.

RAIS KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI.

Posted on Sep 10, 2012 | No Comments

Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake  ni  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala  baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Nyuma yao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha anayefuatana na  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala Septemba 10, 2012  baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo   Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia  ni  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akisoma hotuba yake kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) kilichoko Kunduchi jijini Dar es salaam, pamoja na kuzindua kozi ya kwanza ya mwaka mmoja. Walioketi karibu yake  ni  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala.
Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akipozi na wanachuo wa kozi ya kwanza ya mwaka mmoja katika Chuo cha UIinzi (National Defence College) alichofungua rasmi Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam.
(PICHA NA IKULU).

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru