photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > KAULI YA JAMES MBATIA KUHUSU MAUJI YA IRINGA.

KAULI YA JAMES MBATIA KUHUSU MAUJI YA IRINGA.

Posted on Sep 6, 2012 | No Comments


Wakati bado kuna sintofahamu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia (pichani), amewaonya Wanasiasa na Viongozi wa dini kutotoa kauli nzito ambazo zinaweza kuhatarisha amani.
Pia, Mbatia pamoja na Viongozi wengine wa vyama vya siasa nchini vimemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kukaa kikao cha dharula ili kujadili suala hilo kwa undani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mbatia alisema “Tunaungana kulaani kwa nguvu zote, lakini hatutaki kuishia kulaani bali tumejipanga sisi Wanasiasa kukutana na Waziri Mkuu pamoja na Msajili wa vyama, Waziri Nchimbi na timu yake akiwemo IGP na mawaziri wengine katika kikao cha dharula”
Alienda mbali zaidi na kusema Wanasiasa na Viongozi wa dini wametoa kauli nzito nzito juu ya tukio husika lakini zinaweza kuipeka nchi pabaya.
Badala yake alishauri nchi itulie katika kipindi hiki na Wanasiasa hao na Viongozi wa dini kuacha kutoa kauli hizo kwa sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru