NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA AFANYA ZIARA TAZARA
Posted on
Sep 6, 2012
|
No Comments
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyenyoosha mikono)akiteta jambo na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na Baadhiya Wakurugenzi wa TAZARA wakati wakimsubiri Naibu Waziri Mkuu waChina, Mhe.Hui Liangyu aliyekuwa na ziara ya saa moja katika taasisiya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA. Kulia kwa Waziri niKatibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo na Kushoto kwa
Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi,Bw. John Mngodo.
Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi,Bw. John Mngodo.
Waziri wa Uchukuzi akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu katika Station ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Naibu Waziri Mkuu wa China alikuwa na Ziara yakuangalia Namna Station hiyo inavyofanya kazi. Serikali ya Chinaimetuma wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti wa namna yakuboresha Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu (Mwenye Tai yaBluu),akisalimia na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Reli yaTanzania na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasilini kwenye stesheni hiyo.
Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu (wa saba kutokakushoto),akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara yaUchukuzi, baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Reli yaTanzania na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasili katika station hiyo leo asubuhi.
Mr. Miao Zhong mmoja wa watafiti waliotoka China akimuonyesha Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu(kulia kwa aliyejishikajicho) njia ya reli ilipoanzia kwa upande wa Tanzania. Naibu Waziri
Mkuu wa China alikuwa na ziara katika Mamlaka hiyo leo asubuhi.
Waziri wa Uchukuzi akisisitiza jambo kwa waandishi waHabari (hawapo pichani),kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara yaUchukuzi, Mhandisi Omar Chambo na Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu
Wa Wizara ya Uchukuzi, Bw.John Mngodo.
Wa Wizara ya Uchukuzi, Bw.John Mngodo.