SIRI YA OPERETION KAMATAKAMATA YA TANESCO NI HII HAPA..
Posted on
Sep 9, 2012
|
No Comments
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutaka isitishe utekelezaji wa malipo ya Sh96 bilioni kwa Kampuni ya Kufua Umeme ya Dowans kutokana na kuvunja mkataba wa kibiashara kinyume na sheria.
Kufuatia uamuzi huo, Tanesco sasa inatakiwa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha ambacho kwa ujumla kinaliongezea shirika hilo mzigo wa madeni. Tanesco kupitia mawakili wake Rex Attorneys iliwasilisha mahakamani hapo maombi mawili; kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama hiyo iliyotolewa Septemba 28, 2011 na kuomba kusimamishwa kwa utekelezwaji wa hukumu hiyo.

Katika hukumu ya awali iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, mahakama hiyo ilikubali maombi ya Tuzo kwa Dowans iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), Novemba 15, 2010.
ICC iliamuru Tanesco kuilipa Dowans fidia ya Dola za Marekani billion 65,812,630.03, kutokana na kuvunja mkataba wa kibiashara kinyume cha sheria.
Mahakama Kuu Tanzania ilikubaliana na tuzo hiyo na kuipa kampuni hiyo nguvu ya kisheria.