JACK WOLPER ATWAA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL
Posted on
Oct 27, 2012
|
No Comments
Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Chidy Benz akikamua jukwaani hapo.
Omm Dipoz akizungumza na mashabiki zake jukwaani.
Dogo Asley akiwajibika.
Awali jana mchana hawa ni baadhi ya watoto wakichezeshwa ukumbini hapo.
Mmoja wa watoto waliofika Dar Live mchana akikabidhiwa baiskeli baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa kuruka kamba.
Mchekeshaji maarufu Mtanga, akizungumza na mmoja wa watoto ndani ya Dar Live.
Sehemu ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo.
---
MSANII
wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia
leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa
wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala
jijini Dar es Salaam.
Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima.
Usiku
wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa
Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya
watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.Habari/Picha: Musa
Mateja/GPL