SIMBA YAITUNGUA AZAM FC YA CHAMAZI MAGOLI 3-1 UWANJA WA TAIFA
Posted on
Oct 27, 2012
|
No Comments
Beki
wa timu ya Simba Shomari Kapombe akimiliki mpira mbele ya Ibrahim
Shikanda mshabuliaji wa timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya
Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es
salaam, mpira umekwisha Simba imeibuka kwa ushindi mnono wa magoli 3-1
dhidi ya Azam FC ambayo yamefungwa na Felix Sunzu kwa kichwa na
Emmanuel Okwi la pili na la tatu lililofungwa kipindi cha pili dakika za
mwanzomwanzo, goli la Azam limefungwa na mshambuliaji John Boko.
Huko Arusha timu ya Yanga ilikuwa
mgeni wa timu ya JKT Oljoro ya huko katika mchezo uliofanyika kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo Yanga imeibuka na ushindi wa goli
moja lililofungwa na Mchezaji Mbuyu Twite
Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kupata goli la pili katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu aAzam FC wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Azam wakiishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Simba uwanja wa Taifa jioni hii.