photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MGOGORO WA ZIWA NYASA TANZANIA TUNAWEZA KUFANYA KILE IRAN ALICHOKIFANYA DHIDI YA AZERBAIJAN

MGOGORO WA ZIWA NYASA TANZANIA TUNAWEZA KUFANYA KILE IRAN ALICHOKIFANYA DHIDI YA AZERBAIJAN

Posted on Oct 9, 2012 | No Comments


Na Yericko Nyerere
Katika hali inayoonyesha kuwa Malawi wanakataa suluu ya mgogoro wa kihistoria wa mpaka wa Tanzani na Malawi kule ziwa Nyasa, ni kuwa hivi sasa wenzetu wamesusia vikao vya majadiliano ya kidiplomasia.
Ususiwaji huu umekuja katika kipindi ambacho hoja za nguvu kwa kila upande zikimiminika mezani pa wanaupano pasina kificho wala ghiriba kwa pande yoyote,
Kile nilichokiona pale Lilongwe na Mzuzu kilinipa matumaini makubwa ya hitimisho la mzozo huu kwa upande wa Tanzania uliowakilishwa na ujumbe mzito na maridhawa ulijiandaa vyema na ulikuja na nyaraka zote nyeti na zakale (za mjerumani) Ndugu Bernad Membe waziri wa Mashauri ya kigeni alikonga nyoyo za wajumbe wa tz huku nyoyo za Wanyasa zikiduwaa bila kuamini kama Tanzania inazo nyara muhimu na za kale kiasi hicho,
Vivyo hivyo jopo la wanasheria nalo lilijipambanua vya kutosha na kuonyesha dhahiri mgogoro huu unaelekea ukingoni,
Kwa ujumla jopo lote toke tz lilitumika kama ilivyokusudiwa, na wajumbe waligawanywa katika makundi makuu matatu, 1. Wanadiplomasia, 2. Wataalamu wa Ramani na 3. ni Wanasheria.
Baada ya kikao cha Mzuzu maazimio yalikuwa ni makutano ya Dar es Salaam mnamo tarehe 10-14/9/2012, lakini katika hali ya kushangaza rais Banda ametoa amri ya nchi yake kujitoa katika majadiliano hayo,
Hoja yake kuu anataka Tanzania itoe maelezo "kwanini imefanya mapitio/imechora upya ya ramani ya nchi wakati tupo kwenye mgogoro?"
Hoja hiyo inajibiwa na Tanzania kwa ufasaha kabisa kuwa "Uchoraji huo hauhusiani na uwepo wa mgogoro huo bali Tanzania imeongeza idadi ya mikoa na wilaya zake hivyo kama taifa huru imeamua kuainisha maeneo hayo katika ramani ya nchi yetu sambamba na mipaka ya NCHI"
Lakini hata hivyo bado Malawi imesusia majadiliano na Tarehe 8/10/2012 imetangaza kuendelea na utafiti wa mafuta na gesi katika eneo linalogombewa.
Bado nafasi ya kidiplomasia ipo, Ninawasihi Malawi na Joyce Banda warejee kwenye meza ya majadiliano, kama sisi wawili tumeshindwana tutafute msuluhishi atakae aminiwa na wote, na ikishindikana twende UN.
Kama juhudi zote zikishindikana kwakuwa Malawi wanaonekana wanachembe ya shinikizo la kimagharibi basi njia nyingine ni kutazama historia zenye kufanana na utatuzi wake mfano mzuri ni mgogoro wa Caspian sea kati ya Iran na Azerbaijan
Mgogoro kama huu ulitokea huko Caspian sea kati ya Iran na Azerbaijan mwaka 2001, Utashangaa kuona jinsi Mwingereza anavyoshirikiana na Mmarekani kwenye mambo ya mafuta. Kama ilivyo Malawi sasa kampuni ya utafiti inatoka Uingereza ila masuala ya usalama yamesimamiwa na Mmarekani.
Katika mgogoro huo Iran iliamua kuweka gunboat na kusema haitambui hiyo mikataba iliyoingiwa na Azerbaijan na hata kuifukuza BP kufanya kufanya utafiti hapo.

Rejea hapo chini:

 By Craig Nelson in Moscow
12:01AM BST 29 Jul 2001
THE rush to exploit the oil riches beneath the Caspian Sea is threatening to turn violent after an Iranian patrol boat chased two British Petroleum vessels from a disputed exploration site off Azerbaijan last week.
A gunboat from the Islamic republic intercepted the British oil company's ships while the crews were conducting a marine survey 95 miles east of Baku, Azerbaijan's capital.
The Iranians ordered the exploration team out of the area - an offshore oilfield claimed by both Iran and Azerbaijan. Iran's oil ministry further stoked tensions by announcing that all contracts to prospect in the contested area were invalid and warning oil firms against any plans to drill there, the Itar-Tass news agency reported from Teheran.
The move marks the growing militarisation of this corner of Asia, which has become increasingly tense following the discovery of vast oil reserves. The 700-mile-long Caspian contains six oilfields, most of which have not been developed. Its total possible reserves could be many times the proven deposits of up to 34 billion barrels.
Last month, Washington - which sees the region as a important new source of oil for the United States - delivered two patrol boats to the Azerbaijan government to help monitor its borders. The US State Department said the vessels were "non-lethal" and plans to send more.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru