MTETEZI WA ELIMU PAKISTAN ANUSURIKA KIFO
Posted on
Oct 10, 2012
|
No Comments
Malala Yousafzai,
Madaktari
nchini Pakistan wamefanikiwa kutoa risasi kichwani mwa msichana wa miaka
14 mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Hii ni baada ya msichana huyo kushambuliwa kwa
kupigwa risasi hapo jana alipokuwa akitoka shuleni Kaskazini Magharibu
mwa eneo la Swat.
Taarifa kutoka kwa madakatari wake zinaeleza kuwa hali ya msichana huyo iko shwari kwa sasa.
Malala alituzwa tuzo la nobel kutokana na juhudi
zake za kupigania haki ya elimu kwa wasichana wa Taliban ambao kwa
mujibu wa desturi za kitaliban haswa katika eneo la Swat walikuwa
hawaruhisiwi kupata elimu
Ndugu yake aliambia BBC kuwa, madaktari,wangali wanatafakari ikiwa wampeleke nje kwa matibabu zaidi.
Kundi la Taliban lilisema lilihusika na shambulizi hilo.
Malala Yousafzai aliandika kitabu cha kumbukumbu
zake binafsi kwa niaba ya BBC miaka mitatu iliyopita wakati eneo la
Swat lilikuwa linadhibitiwa na kundi laTaliban.
Wanasiasa nchini Pakistan, walilaani shambulizi hilo huku Marekani ikilitaja kama kitendo cha uoga