photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SENTENSI 3 ZA KAULI MPYA YA TPI KUHUSU ISHU YA DAWA FEKI ZA ARV.

SENTENSI 3 ZA KAULI MPYA YA TPI KUHUSU ISHU YA DAWA FEKI ZA ARV.

Posted on Oct 23, 2012 | No Comments


Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi

Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Tanzania Pharmacetical Industrial (TPI) kimesema Serikali inabidi iharakishe uchunguzi kuhusu mtu aliyeingiza nchini dawa bandia ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi iitwayo TT-VR 30 ili kuondoa wasiwasi ulioenea kwa watumiaji.
Mkurugenzi mtendaji wa TPI Ramadhani Madabida amesema uchunguzi wa awali unaonyesha serikali inamfahamu mtu alieingiza hizo dawa Tanzania, zilipotoka na tarehe ya kuingizw hivyo kuharakishwa kwa mchakato huo kutakomesha mizengwe ya baadhi ya wawekezaji kutoka nje kutaka kuchafua ubora wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.
Tayari serikali imewasimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa nchini MSD Joseph Mgaya pamoja na mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na afisa udhibiti ubora wa MSD kutokana na kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo bandia ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru