SERA YA NJE YA MAREKANI YAZIDI KUMTAFUNA OBAMA DHIDI YA MPINZANI WAKE ROMNEY.
Posted on
Oct 23, 2012
|
No Comments
Mitt Romney na Rais Barack Obama.
Rais Obama na mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republican wamepambana kwa hoja katika awamu ya tatu na ya mwisho katika mji wa Boca Raton-Florida, wakati zimebakia siku chache kufanyika uchaguzi.
Sehemu kubwa ya mdahalo wao wa muda wa saa moja na nusu ilikuwa juu ya sera ya nje ya Marekani kuhusiana na Iraq, Afghanistan, Libya, Iran na Mashariki ya Kati.
Mgombea urais wa chama cha Republican Romney amesema sera ya Obama ya kutumia nguvu dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wenye itikadi kali haitoshi katika kukomesha hatari ya siasa kali.
Romney amempongeza Rais Obama kwa kumzima Osama
Bin Laden na kwa kuwakabili viongozi wa al-Qaeda, lakini Romney
ameeleza kuwa Marekani haiwezi kuondokana na hatari hiyo kwa njia ya
kuua.
Amesema Marekani inapaswa kufanya zaidi ili kuwafanya watu katika nchi za kiislamu wapinge itikadi kali.
Akijibu hoja hiyo Rais Obama amesema mpinzani wake, Romney anafanya makosa katika kila suala linalohusu sera ya nje.
Obama amesema ameifanya dunia iwe na usalama zaidi tokea alipoanza kuwa Rais wa Marekani miaka minne iliyopita.