photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SPIKA MAKINDA ALAZIMIKA KUAHIRISHA BUNGE KUTOKANA NA IDADI NDOGO YA MAHUDHURIO YA WABUNGE.

SPIKA MAKINDA ALAZIMIKA KUAHIRISHA BUNGE KUTOKANA NA IDADI NDOGO YA MAHUDHURIO YA WABUNGE.

Posted on Oct 30, 2012 | No Comments

Kikao cha bunge chaanza Dodoma  na Spika wa Bunge akiingia ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Spika Anne Makinda akiahirisha kikao cha Bunge kufuatia kuwepo kwa mahudhurio madogo ya Wabunge.
Muonekano wa siti za Waheshimiwa Wabunge mjini Dodoma leo zikionekana kuwa wazi.
Na.Mwandishi wetu Dodoma.
Kikao cha Bunge kimeanza leo mjini  Dodoma huku  mawaziri wakpigwa maswali makali na wabunge waliohudhuria kwa idadi ndogo ukilinganisha na vikao vingine vya Bunge.
Wabunge walianza kuuliza maswali wabunge katika wizara za Tamisemi, Fedha,Maji, Nishati na Madini, ofisi ya rais katika kitengo cha Mkurabita na hatimaye walimalizia katika wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Spika wa bunge alikuwa kivutio kwa kusuka mtindo wa pekee  na kuwakonga mioyo wabunge wengi waliohudhuria kikao cha leo.
Spika naye hakusita kumpongeza waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuanza kwa huduma ya safari ya Treni maalumu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Baadaye Spika alihairisha kikao cha bunge baada ya kuwepo kwa mahudhurio madogo ya wabunge mara baada ya waziri wa  Fedha na Masuala ya Uchumi kuwasilisha bungeni  Azimio la Kuridhia  Marekebisho ya pili ya mkataba wa  Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya na nchi za Afrika.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru