photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > VURUNGU ZA WAISLAM MBAGALA KATIKA PICHA

VURUNGU ZA WAISLAM MBAGALA KATIKA PICHA

Posted on Oct 12, 2012 | 1 Comment

Vurugu zilizofuatia mtoto anayeitwa Emanuel Josephat(14)’ kukojolea msaafu (Quran) zimechukua sura mpya baada ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislam kukusanyika na kushinikiza mtoto huyo aachiwe na polisi ili wamuue.
Waumini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma moto kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, wakaharibu Kanisa la Anglican, wakavunja vioo vya kanisa la Wasabato, na kuchoma moto Tanzania Assembly of God (TAG), la Mbagala Kizuiani na kuchukua vifaa vya muziki vya kanisa hilo na kuvichoma moto hadharani.
Awali waumini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi cha Maturubai, Mbagala Kizuiani wakitaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa polisi aachiwe na Polisi walipokataa matakwa yao ndipo vurugu hizo zilipoanza.
Chanzo cha tukio hili ni mabishano baina ya watoto wawili, Emmanuel Josephat, na mtoto mwingine wa Kiislam.
Watoto hao walikuwa wakibishana kuhusu imani na dini ambapo mtoto wa Kiislam alimwambia Emmanuel kuwa, “Quran ni kitabu kitakatifu, endapo utafanya chochote kibaya juu yake basi utadhurika, waweza kuwa kichaa”.
Hapo ndipo Emmanuel alipoamua kuikojolea Quran ili kuona kama atakuwa kichaa.
Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.
Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.
Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.
“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa!?” alihoji mmoja wa viongozi hao

vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 6 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Baadhi ya wafanya furugu wakipambana na polisi
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji katika eneo la Mbagala Kizuiani katika harakati za kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kukojolewa na mtoto Emmanuel Josephat. Picha na Happy Mnale
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 00 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Hamis Salum, baba wa mtoto ambaye Quran yake imekojolewa akiongea na vyombo vya habari
kanisa limechomwa Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Mojawapo ya makanisa yanayosemekana kuharibiwa likiungua moto
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 0 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
FFU wakijiandaa kutuliza fujo
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 1 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Mmoja ya wa waandamanaji akiwa amekamatwa na (FFU)
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 2 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Moja ya gari lililoharibiwa katika vurugu hizo
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 3 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Baadhi ya waandamanaji waliokamatwa wakipandishwa kwenye gari la polisi
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 4 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamekamatwa na polisi
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 5 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 7 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Polisi katika harakati za kuthibiti fujo
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 8 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Baadhi ya watuhumiwa wakipandishwa kwenye gari la polisi
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 9 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Polisi wakiwavusha baadhi ya watuhumiwa waliowakamata kwenye mfereji
vurugu mbagala baada ya kukojolea msaafu quran 10 Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Mmoja wa watuhumiwa akiwa amekamatwa na polisi
gar Baadhi ya Waislam waidai polisi mtoto aliyekojolea msaafu ili wamuue; picha zaidi za vurugu Mbagala
Moja ya magari la polisi yualiyoharibiwa

Comments:1

  1. Sijui ni Mungu yupi ambaye hana nguvu na hata anapotendewa mabaya basi sisi tunakuwa na nguvu kuliko yeye kisha kulipizia Kisasi. Kama Taifa lazima tuondokane na ujinga huu. Dini inapotumika kuligawa Taifa na kulisambalatisha taifa hapo dini hiyo au watu wake wahusika hawapaswi kubaki kama walivyo.

    ReplyDelete