WATU WANANE WAKAMATWA NA VIFAA VYA KULIPULIA MABOMU KANISANI BUKOBA
Posted on
Oct 8, 2012
|
No Comments

Taarifa nilizozipata kutoka Bukoba ni kwamba,watu wanane
wamekamatwa wakiwa nje ya kanisa katoliki mjini Bukoba wakiwa na vifaa ambavyo
uchunguzi wa awali ulionesha kuwa ni vya mlipuko.
Katika kanisa hilo ndipo misa
ya shukrani iliyohudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter
Pinda,ilifanyika katika kanisa la Cathedral ambapo ndipo mwili wa Cardinal
Rugambwa ulizikwa rasmi jumamosi.
Watu hao wameshikiliwa kituo cha polisi kwa
uchunguzi na mahojiano zaidi.