photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> HUENDA UINGEREZA IKAJITOA UMOJA WA ULAYA.

HUENDA UINGEREZA IKAJITOA UMOJA WA ULAYA.

Posted on Nov 2, 2012 | No Comments

 Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Nick Clegg ameonya kwamba wabunge pinzani katika bunge la nchi hiyo huenda wakaiona Uingereza inajitoa kwenye Umoja wa Ulaya.
 Clegg kiongozi wa chama cha Kiliberali kinachounga mkono Umoja wa Ulaya ameyatoa matamshi hayo baada ya Waziri Mkuu David Cameron, kushindwa vibaya bungeni kuhusu mpango wake wa kutaka kupunguzwa kwa bajeti ya Umoja wa Ulaya.
 Cameron amesema atapambana kuhakikisha matumizi katika bajeti yanapunguzwa. Aidha, anataka bajeti ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya iongezeke sambamba na mfumuko wa bei.
Habari hii ni kwa hisani ya idhaa ya Kiswahili ya DW.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru