MSANII WA TAARAB WA KUNDI LA TOT PLUS, MARIAM KHAMIS MAARUFU KAMA PAKA MAPEPE AMEFARIKI DUNIA
Posted on
Nov 13, 2012
|
No Comments
Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam Khamis maarufu
kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa
jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam mara tu baada ya kujifungua .
Mariam Khamis umauti umemkumba akiwa anaimba kundi la TOT plus lakini enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab likiwemo East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.
Khamis Muhidini Shomary baba wa marehemu amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa hapo kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.