ROBERTO MANCINI NA KAULI YAKE KUHUSU GAME YA MAN CITY NA AJAX.
Posted on
Nov 5, 2012
|
No Comments
.
Manager wa club ya Manchester
city Roberto Mancini amekubali kwamba game yao ya novemba 6 2012 na Ajax
ndio nafasi pekee waliyonayo kwenye champions league na kuhusu majeruhi, amesema wako wachezaji wengine wa kikosi chake ambao wanaweza kucheza vizuri tu.
Mancini alikasirika baada ya
mwandishi kumuuliza swali, kwa sababu msimu uliopita alisema kulikuwa
na uwezekano mkubwa wa kushinda Champions league na leo anasema novemba 6
wana nafasi pekee ya champions legue, Mancini
alikasirika na hakujibu swali bali akasema kwa nini unaniuliza mambo ya
msimu uliopita, ya mwaka uliopita, ya mambo yaliyopita.
Namkariri akisema “miaka 15
kabla ya mimi kujiunga na Man city, ilikua haijawahi kushinda kombe, ila
nilipoingia imeshinda makombe matatu ndani ya miaka miwili, hivyo
usiendele kuwakosea watu heshima”