photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SABABU KUU YA AJALI ZA BARABARANI TANZANIA NI HII HAPA!!!

SABABU KUU YA AJALI ZA BARABARANI TANZANIA NI HII HAPA!!!

Posted on Nov 29, 2012 | 1 Comment


Click image for larger version. 

Name: AJALI YA GARI T 601 APK BARABARA YA KOROGWE MORO MISITU PIX NO 2.JPG 
Views: 0 
Size: 343.4 KB 
ID: 72655Pamoja na uzembe wa madereva kuchangia katika asilimia kubwa sana ya ajali za magari barabarani,na kusababisha vifo vya maelfu ya raia wasio na hatia yoyote sasa tunakuletea sababu moja wapo ya msingi ya kukithiri kwa ajali siku za hivi karibuni:
madereva wengi sana wanaojifunza gari mijini(dar-arusha-tanga)wakishapata lessen tu,huwa na mzuka wa kukata masafa marefu na gari zao au za kuazima,kimatembezi,au kwa shida nyengine yoyote ile!!bila kuweka katika akili zao kuwa barabara zote zinazokwenda mikoani huwa zinamisukosuko ya aina mbali mbali!!
1:inahitaji uwe mzoefu wa hali ya juu katika ku overtake
2:inatakiwa ujuwe sehemu za ku overtake au kuto overtake ili kujiepusha na ajali

 
3:uwe na uvumilivu wa kukwepa makosa ya madereva wengine,ili kujiepushia ajali
4:masafa ya km200-1200km si sawa na 20km au 15 km,safari ndefu zinataka angalau ukae kushoto hata mara mbili

Click image for larger version. 

Name: 5.jpg 
Views: 0 
Size: 165.6 KB 
ID: 72658
barabara zetu za mikoani zina changamoto mbali mbali unapoendesha gari majira ya usiku huwezi kuyaepuka kama wewe si dereva mzoefu wa njia hizo!!!
1:kuna gari nyingi usiku huwa zinatembea na taa moja tu,unaweza ukadhani pikipiki ukiibana imekula kwako!
2:kuna matreckta yanavuta matela nyakati za usiku bila kuwa na ishara yoyote,na ajali nyingi hutokea hapo!!
3:kuna madereva wanaowasha taa zenye mwanga mkali bila kuzizima,hivyo kukusababishia kupata ajali!

Click image for larger version. 

Name: DSC2936-web60-copy.jpg 
Views: 0 
Size: 39.8 KB 
ID: 72660
ninachopenda kuwaeleza madereva wa mjini muliokuwa hamuna idea na barabara za mikoani,kabla ya kuchukua maamuzi ya kuhatarisha maisha yako au ya familia yako,unapotaka kukata masafa marefu ya mikoani hali ya kuwa huna idea ya marabara za huku,ajiri dereva akuendeshe angalau tripu mbili au tatu,upate uzoefu,na muchangie katika kutupunguzia ajali,ambazo sisi wakazi wa mikoani tunaona madereva wengi wanaotusababishia ajali nyingi hutokana na kutokuwa wazoefu wa njia zetu!!!!!!

Comments:1

  1. Kweli kabisa hajali nyingi pia zinachangiwa na madreva wazembe.

    ReplyDelete