LOWASSA ATAKA MFUMO WA ELIMU UFUMULIWE
Posted on
Dec 12, 2012
|
No Comments
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu,
Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili
kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla
mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi
za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.Lowassa alisema hayo
jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini
kwake jijini Dar es slaam.‘’Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa.
kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia
mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu
hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya
kuhusu mfumo wa elimu yetu.’’alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa
kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. “Tume
hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa
unaendana na wakati,”Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa
zikifanya hivyo.“Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa
kama inaendana na changamoto za karne ya 21,” alisema.Kumekuwa na malalamiko
mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini,
haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni
pamoja na kujiajiri.Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali
ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya
nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika
kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma,
CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu
nchini.‘’Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio
makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto
zake’’alisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni
ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi
vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu. Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na
wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili
kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa
anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?.
Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea
Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?