NAULI ZA KWENDA MIKOANI ZAPANDA KINYEMELA
Posted on
Dec 8, 2012
|
No Comments
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za
mabasi wamepandisha nauli za mabasi kinyemela, licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kuwapiga marukufu. abiria mbalimabali
wamekuwa wakitozwa kiwango cha juu tofauti na kile kilichowekwa na SUMATRA na
kusababisha usumbufu kwa abiria. Uchunguzi ulifanywa na kugundua kuwa nauli
kutoka Dar kwenda Mwanza imefikia kiasi cha sh 50,000/= badala ya sh 40,000/=,
kwenda Iringa imepanda hadi sh 25,000/= badala ya sh 18,000/=, kwenda Masasi
imefikia sh 25,000/= badala ya sh 22,000/=, Tunduma nauli kwa sasa ni sh
40,000/= badala ya sh 35,000/=. Imeelezwa kuwa wafanyakazi wa kampuni
mbalimbali za mabasi wanakuwa na vitabu viwili vya kakatisha tiketi, abiria
AKILALAMIKA KUWA NAULI KUBWA HUBADILISHA KITABU NA KUMKATIA TIKETI NYINGINE KWA
BEI HALISI (ukiwabana wanakutoza nauli halisi) ila kama hujui viwango vya nauli
hizi utatoa kiasi wanachotaka wao. Kwahiyo kuweni macho wadau mnaotumia usafiri
huu muhimu wa mabasi yaendayo mikoani, hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
NAKUTAKIENI SIKUKUU NJEMA "X-MAS NA MWAKA MPYA".