ORODHA YA AHADI ZA KIKWETE KWA WANANCHI 2010-2015 NA MAHALI ALIPOZITOA
Posted on
Dec 11, 2012
|
No Comments
Kujenga reli mpya kutoka
Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
Mkoa wa Tanga kuwa Jiji
la Viwanda - Tanga mjini
Tabora kutumia maji ya
Ziwa Victoria - Igunga
Kulipa madeni ya chama cha
Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
Kumaliza migogoro ya
Ardhi nchini - Dodoma
Wakulima kuacha kutumia
jembe la mkono - Dodoma mjini
Kuwapatia trekta wakulima
- Kata ya Mrijo, Dodoma
Wananchi kutoondolewa
kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
Kujenga Uwanja wa Ndege
Misenyi - Kagera
Kupanua Uwanja wa Ndege
Bukoba - Bukoba Mjini
Kujenga uwanja wa ndege
mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
Mtukula kupatiwa umeme
kutoka Uganda - Kagera
Mikoa ya Kagera, Kigoma,
Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
Kuimarisha Takukuru kwa
miaka mitatu - Kagera
Hukumu kwa waliopatikana
na hati ya kuua albino - Mbeya
Kununua meli kubwa kuliko
MV Bukoba - Kagera
Kuanzisha benki
ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
Serikali kuvisaidia vyama
vya ushirika - Mwanza
Kuimarisha usalama Ziwa
Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana
na wahalifu - Mwanza
Wilaya ya Geita kuwa
hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
Kulinda muungano kwa
nguvu zote - Pemba
Kuwajengea nyumba
waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
Kununua meli mpya kubwa
Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
Kujenga bandari Kasanga –
Rukwa
Kumaliza tatizo la walimu
miaka mitano ijayo - Songea
Kufufua mgodi wa makaa ya
mawe Kiwira - Mbeya
Kuzuia hatari ya kisiwa
cha Pangani kuzama - Tanga
Kununua bajaji 400 kwa
ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
Kujenga barabara yenye
kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na
barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
Kumaliza tatizo la maji
katika wilaya ya Same - Same Mjini
Kuboresha barabara za
Igunga - Tabora
Kusambaza walimu 16,000
katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
Kununua vyandarua viwili
kwa kila kaya - Mbeya Mjini
Kuzipandisha hadhi
hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
Kulinda amani nchini kwa
kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
Kulinda haki za walemavu
- Makete
Kujenga baabara ya Njombe
- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
Kujenga barabara Musoma –
Mto wa Mbu Arusha - Arusha
Kuanzisha jimbo la
Ulyankulu- Shinyanga Mjini
Kujenga barabara ya lami
Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
Kukarabati barabara ya
Arusha Moshi - Arusha Mjini
Kuboresha barabara ya
Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
Kuwafidia wanakijiji
ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
Vijiji vyote vilivyoko
kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria -
Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
Tatizo la umeme kufikia
kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
Kukopesha wavuvi zana za
kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
Kuwapatia maji wakazi wa
Wilaya ya Longido - Longido
Kujenga barabara ya lami
kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
Utekelezaji wa mpango wa
maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao
vizuri - Mbulu mkoani Manyara
Kusambaza maji nchi nzima
- Babati vijijini
Kusambaza umeme, utoaji
wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa
wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
Kuongeza mara tatu idadi
ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha -
Iringa
Kuhakikisha Isimani
inapata maji ya uhakika - Iringa
Kuiwekea lami barabara
inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko
zote Tanzania - Iringa
Kulinda usalama wa
wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
Kutokomeza malaria 2015 -
Bunda, mkoa wa Mara
Kuwapa wanawake nafasi
zaidi - Kilolo, Iringa
Ahadi kuisadia Zanzibar
kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
Kuipandisha hadhi
hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
Kuisaidia Zanzibar kila
panapohitajika msaada - Kibandamaiti
Serikali kujenga upya
bandari ya Mbambabay - Ruvuma
Ununuzi wa Meli mpya
yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
kufufua chama kikuu cha
ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
Ahadi Rais wa Marekani
Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
Ahadi hakutakuwa na
umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
Mtwara kuwa mji wa
Viwanda – Mtwara
Ahadi ujenzi wa kwanda
cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
Hospitali ya Tumbi kuwa
ya mkoa - Kibaha
Halmashauri ya manispaa
ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
---2005 Alikuja na Maisha bora kwa kila Mtanzania,hili halina ubishi lilikuwa ni changa la macho kwa Watanzania,Kama haitoshi akasema anawajua kwa majina wala rushwa,lakini hatuoni hata mmoja aliyemchukulia hatua===hii ni kutaka sifa na popularity.
---Juzi amekuja na mpya ya kumpatia kila mwanafunzi Computer ambayo iko connected kwa internet, it's high time now kwa watanzania kuhoji uwezo wa RAIS wetu,ni kwamba anafanya Wa Tanzania ni wapumbavu sana kiasi kwamba hawawezi ku reason kuwa hilo sual haliwezekani???
Hata kwa wanafunzi tu wa vyuo vikuu hilo suala halitekelezeki leo anatuambia ataanza na shule za msingi,umeme ni tatizo..hivi jk anajua kuwa its only 10% ya wa Tanzania wana access na umeme na 0.05% ya watanzania ndo wanaweza kutuima computer na wana access na internet,hata kwa nchi ambazo zimeendelea kuzidi sisi hilo suala halipo,,yeye anataka kuhadaa Wa Tanzania aili aendelee kubaki madarakani!!!!!me nadhani pia JK na uwezo mdogo sana wa ku reason ndo maana hata hafikirii kuwa suala kama hilo watu wenye akili timamu hawawezi kusadiki,inahitaji mtu mwenye akili za mwenda wazimu kuamini ahadi kama hizo.
----WITO WANGU
Nawaomba wana JF wooote..mu influence watu wenu wa karibu wasimchague JK na CCM yake,watatoa ahadi nyingi sana,watasema watajenga fly over,watasema watajenga majumba angani--->tuwapuuuze na ahadi zao hizo...tuwaulize kati ya zile walizoahidi 2005 ni ngapi wametekeleza mpaka tuwape ajira nyingine kwa miaka mitano!!!!!!
Watakuja na gia ya kuwa wamejenga DOdoma University,tuwapuuze pia kwa sababbu kwanza ulikuwa ni ukumbi wa bunge wa zamani (chimwaga),halafu huo ni wajibu wake...tuipuuzie kete ya kipuuzi kama hii.
SAY NO TO CCM-----SAY NO TO JK-----WANYIMENI KURA