DR DALALY KAFUMU SIUTAKI UBUNGE.. NALAZIMISHWA
Posted on
Jan 10, 2013
|
No Comments
Aliyekuwa
Mbunge wa Igunga,Dr.Dalaly Peter Kafumu, amedai kuwa kwasasa yeye hataki Ubunge
lakini CCM inamlazimisha kukata na kuishughulikia rufaa yake dhidi ya kuvuliwa
Ubunge huo na Mahakama Kuu. Nikizungumza naye hivi punde, Dr.Kafumu
ameilalamikia CCM kwa kuwakosesha Mbunge wana-Igunga kwa kung'ang'ania rufaa ya
Ubunge isiyo na tija.
'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.Sitaki hata kusikia Ubunge wala nini sijui. Washauri Viongozi wetu wakubali Jimbo litangazwe wazi na uchaguzi ufanyike upya ili wana-Igunga wawe na Mbunge. Nilishakubali matokeo ya Mahakama.' alisema Dr.Kafumu
'Niliandika kuwafahamisha viongozi wangu. Sasa kwanini hawataki kunielewa? Kwanini wananilazimisha? Kwanini wanang'ang'ania jambo hili? Hawa watu sijui wakoje?!' alisikika Dr.Kafumu kwa sauti ya kukwazika.
Jambo gani liko nyuma ya Jimbo hili la Igunga?