POLISI WALIOUWAWA KARAGWE: UKWELI HUU HAPA..
Posted on
Jan 10, 2013
|
1 Comment
Kuna taarifa zimekuwa zikizagaa katika vyombo mbalimbali vya
habari juu ya polisi waliouawa huko Karagwe. Ukweli umefichwa kwa maksudi na lawama
zinaelekezwa kwa raia.
Ukweli wenyewe:
Mtu mmoja wa kijiji cha Rugu (iko wilayani karagwe) alikuwa na meno ya tembo; aliamua kwenda maeneo ya benaco (iko wilayani Ngara) kutafuta wanunuzi. Aliwapata watu wawili. Baada ya makubaliano ya kulipwa shs 12m wale wanunuzi walimweleza kuwa kwa kuwa watakwenda usiku na njiani kuna pori la Kimisi watakwenda na mtu wao mwenye bunduki ambaye huwa anawalinda mara kwa mara.
Walipofika Rugu wakauona mzigo, wakaupima na kukuta kilo walizokubaliana ndivyo zilivyo. Mzigo ulipakiwa kwenye gari lao; jamaa hao wakataka kuondoka bila kulipa. Mwenye mali alipouliza mbona hawampi hela yake alijibiwa kuwa 'sisi ni polisi na haya meno ya tembo ni nyara za serilkali, ukileta fujo tutakukamata!' Kwa kuwa walikuwa na bunduki jamaa aliogopa lakini alijitahidi kupambana na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo. Gari lilipoondoka na mzigo jamaa akapiga simu kwa watu walio kwenye stesheni ndogo ambayo ilikuwa lazima gari hilo lipitie akiwaeleza kuwa wamevamiwa na majambazi lakini wamepambana nao na kupasua kioo cha gari, hivyo wajitahidi kulizuia lisipite.
Raia hao walipanga mawe makubwa barabarani na mara gari hilo likaja - kioo kimepasuliwa na halina namba. Gari liliposimama raia wakaanza kuwahoji wanakotoka na wanakokwenda na walifuata nini. Ikabidi kichapo kitembee kidogo. Jamaa kuona kichapo kinazidi ikabidi waseme kuwa wao ni polisi na kuna mhalifu walikuwa wamnamfuatilia. Lakini raia wakaona hao polisi mbona hawawahamu? Raia waliamua kupiga simu kwa OCS wa kituo cha karibu (Chanyamisa) akawajibu kuwa hana taarifa zozote na watu hao; wakapiga simu kituo cha Omukaliro, OCS akawajibu kuwa hana taarifa;.
Walipiga simu polisi wilayani lakini jibu likiuwa ni hilohilo! Hao Polisi-majambazi kuona hivyo yule aliyekuwa na bunduki akafyatua risasi hewani raia hawakuogopa wakataka wamkamate, akapiga risasi nyingine ikampiga kijana mmoja kwenye mkono!. Hapo ndipo raia waliona kuwa kumbe hawa tukiwalegezea watatuua.
Kichapo kikaendelea lakini aliyekuwa na bunduki alikimbia baada ya kufyatua risasi nyingine. Hao wawili waliobaki walipigwa hadi kufa!
Raia waliamua kulitia gari moto, wakati likiendelea kuuungua walifungua kwenye boot na kukuta meno ya tembo baadhi yakiwa yameanza kuungua kidogo. Huo ndio ukweliBaada ta TBC kutangaza kuwa hao polisi walikuwa wanataka kumkamata mhalifu na raia wakawaua ili wasimkamate, raia wamechukizwa sana uongo huo. Jana usiku kuanzia majira ya saa tatu usiku hadi saa nne na nusu radio moja ya kijamii (Radio fadeco) iliendesha kipindi kwa kuruhusu wananchi kupiga simu kueleza nani alaumiwe kwa mauaji ya hao polisi? Asilimia 99.8 walisema hao hawakuwa polisi bali majambazi tu na kwa kuwa walitumia bunduki kutaka kuwaua raia; basi raia hawakuwa na jinsi bali kuwashughulikia.
Nilimsikia Diwani wa kata ya Kanoni Mh. Sabby B. Rwazo (alikuwa katibu mwenezi wa ccm mkoa kabla ya uchaguzi wa mwaka huu) akieleza kwa uchungu sana jinsi TBC walivyochakachua habari hii. Akiwailisha mawazo ya watu wengi ameitaka TBC kuwaomba radhi wananchi wa Karagwe na kutoa habari iliyo sahihi. Raia wanasema uchakachuaji wa habari hiyo unazidi kuwaondolea imani na serikali; wanajiuliza kwanini ukweli ufichwe? Je kuficha ukweli kutajenga uhusiano mzuri kati yao na polisi? Kumbuka hivi sasa polisi wanawatafuta waliowaua wenzao-ni vurugu tupu!
Wananchi wanauliza maswali haya mazito:

Iweje polisi watoke wailaya nyingine kuja kufanya msako bila uongozi wote wa wilaya ya karagwe kujulishwa (Ngazi ya wilaya hadi kitongoji)?
Kwa kuwa walikuwa tayari wanayo meno ya tembo ni wazi kuwa huyo jangiri walishamkamata - mbona hawakuwa naye? Kwa nini walimuachia?
Hata kama walitaka usakaji huo uwe wa siri kwanza, kwa nini baada ya kupata meno hayo hawakutoa taarifa kwa vyombo vya karibu badala yake waliamua kuondoka nayo?
Kwanini gari la kiraia walilotumia waliamua kuondoa namba?
Kwanini vizuizi vya Benaco, Kimisi na Chanyamisa hawakuwazuia na ilikuwa usiku?
Hakika wananchi wana maswali mengi sana!
hapo hata wakifanyaje lazima wauaji watafutwe, hata kama mapolisi hao walikua majambazi, raia hawakua na haki ya kuwaua kwani sheria haisemi hivyo jambazi auwawe, walitakiwa wawakamte wawapeleke kituono na sheria ichukue mkondo wake. Hii ikiachwa hivyo itasababisha hatari kwa nnchi kwani wananchi wataaendelea kuua askari na iko siku askari ataaua watu wengi,. Tunaamini nnchi yetu inafuata utawala wa sheria, acheni sheria ichukue mkondo wake
ReplyDelete