TAARIFA KUHUSU JAY JAY OKOCHA KUFILISIKA.
Posted on
Jan 6, 2013
|
No Comments
.
Taarifa kutoka kwenye magazeti
manne makubwa ya Nigeria zimeripoti kwamba mchezaji maarufu na wa siku
nyingi nchini humo Jay Jay Okocha anazidi kufilisika kila siku na sasa
anafanya muendelezo wa kuuza mali zake ambazo zilikua kitega uchumi
kikubwa kwake.
Captain huyu wa zamani wa timu
ya taifa ya Nigeria ambae pia alizichezea Bolton Wanderers and Hull City
tayari mpaka sasa ameshaiuza club yake maarufu Nigeria iitwayo Club 10
ambayo ameiuza kwa Producer Don Jazzy ambae ni producer aliewatoa wengi
akiwemo D’Banj, na sasa anafanya kazi na staa Tiwa Savage.
Club 10 ni kiwanja maarufu sana kwenye mji wa Lagos ambapo kimehudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Akon.
Baada ya kuiuza hiyo Club, sasa
hivi anauza nyumba yake nyingine iko Akute, Ogun State ambapo mpaka
sasa imeripotiwa kwamba midfield Maestro yuko tayari kufanya mazungumzo
ya kuanzia N17 million.