photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WATAKAO MALIZA FORM SIX KUPITIA JKT 02 MARCH 2013

WATAKAO MALIZA FORM SIX KUPITIA JKT 02 MARCH 2013

Posted on Jan 7, 2013 | No Comments

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga, kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 1964 kifungu kidogo namba 2b kwenye mabano.
Anawaita (CALL UP) vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria ifikapo tarehe 02 MARCH 2013
Kwa kuanzia utaratibu huo utaanza na vijana 5,000 kutoka shule za Sekondari zifuatazo:
KIBONDO, MUSOMA, KIBAHA, ILBORU, BAGAMOYO, JITEGEMEE, TABORA BOYS, NGAZA, MTWARA GIRLS, IHUNGO, KILAKALA, BENJAMINI MKAPA, MASWA GIRLS, DODOMA, TUMAINI-SINGIDA, GALANOS, ASHIRA, NANGWA-IRINGA, IYUNGA, MPANDA, LINDI, IRINGA GIRLS, KAWAWA-IRINGA, RUHUWIKO-SONGEA.
Maafisa kutoka JKT wataenda katika shule hizo kuanzia tarehe 09 January 2013 kutoa utaratibu wa Mafunzo.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru