HATMA YA WASHUKIWA WA ICC KUGOMBEA KENYA
Posted on
Feb 15, 2013
|
No Comments
Uamuzi unatarajiwa
kutolewa wakati wowote kuanzia sasa kuhusu iwapo wagombe wawili katika
uchaguzi mkuu Kenya Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea
nyadhifa.
Uhuru Kenyatta anawania urais katika uchaguzi mkuu unaowadia katika muda wa wiki mbili zijazo na naibu wake ni William Ruto.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na mashirika yasiyo ya
kiserikali inaendelea katika mahakama kuu mjini Nairobi na inatarajiwa
kutoa uamuzi iwapo mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi juu ya wawili hao
au iwapo itahitaji usaidizi wa mahakama ya juu nchini kufikia uamuzi
kuhusu hilo.
Hii ni wakati zimesalia wiki mbili tu kwa
uchaguzi mkuu kufanyika Kenya na uamuzi huu huenda ukawa na athari kubwa
kwa uchaguzi ujao.
Mahakama inajaribu kuona iwapo Uhuru na Ruto
ikiwa watachaguliwa wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, na
wakati huo huo kukabiliana na kesi inayowaandama katika mahakama ya
uhalifu wa kivita ICC mjini Hague Uholanzi, ambapo wanatuhumiwa kuhusika
na ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.