HUYU NDIYO MWANARIADHA WA SOUTH AFRIKA ALIYEMUUWA MKEWE KWA RISASI
Posted on
Feb 15, 2013
|
No Comments
Mwanariadha Oscar Pistorius alipokuwa katika mashindano ya Olympic mwaka 2012 mjini London.
Mwanariadha na mshindi wa medali za dhahabu wa Paralympic raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amekamatwa nyumbani
kwake mjini Pretoria kwa kosa la kumuua mpenzi wake baada ya kumpiga
risasi moja kichwani na nyingine mkononi , majeraha yaliyopelekea kifo
cha binti huyo.
Chanzo cha Pistorius kumsuti mpenzi wake bado hakijaeleweka, japo fununu za awali zinadai uenda Pistorius alijichanganya na kudhani amevamiwa na mwizi/jambazi kutokana na hali mbaya ya uhalifu anayoikabili nchi ya Afrika Kusini.
Binti huyo Reeva Steenkamp, (30) mwanamitindo alilenga kumsuprise Pistorius kwaajili ya valentine.
Msemaji
wa Polisi aliliambia shirika la habari la Reuters “tumekuta pisto ya
mm9 eneo la tukio, na mtuhumiwa amepelekwa kituoni kwaajili ya utaratibu
mwingine”.
Pistorius mwenye miaka 26 maarufu kama “blade runner” amekuwa ni mlemavu wa kwanza kushiriki
Olympic mbali na mashindano yao maalum ya Paralympic , hukimbia riadha
kwa kutumia vifaa maalum vilivyofungwa miguuni kwake, baada ya kuzaliwa bila miguu yote miwili.
Mpenzi wa Pistorius, Mwanamitindo Reeva Steenkamp aliyepigwa risasi na kupoteza maisha.
Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp November 2012.