KAMA ULIMIS STORI ZA BUNGENI BASI PITIA HUU UKURASA
Posted on
Feb 9, 2013
|
No Comments
Waziri mkuu Mizengo Pinda
amelazimika kuingilia kati mjadala wa wabunge kuhusiana na hoja
iliyotolewa wakati wa mjadala wa mabadiliko ya sheria mbalimbali kuhusu
kutoingiliwa kwa maamuzi yanayotolewa na wazee wa Mahakama kwenye baadhi
ya mashauri yanayohusiana na masuala ya dini ya kiislam ikiwemo ndoa na
mirathi.
Wakati hoja ikiendelea kabla ya
kupitishwa kwake, Waziri mkuu alisema ipo haja ya serikali kuliangalia
upya hilo jambo na kutahadharisha kwamba huo mjadala ungeendelea
ungeweza kuligawa taifa kwa misingi ya udini ishu ambayo ilisababisha
mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema kukifuta hicho
kifungu.
Kwenye sentensi nyingine ni
kwamba ishu ya mitaala ya elimu Tanzania iliendelea kumuandama mbunge wa
kuteuliwa na rais Kikwete, James Mbatia baada ya mbunge wa Nzega Dk
Khamis Kigwangalla kuomba muongozo wa spika kutoa hoja ya bunge
kumwajibisha James Mbatia kwa kuongea uongo bungeni.
Namkariri Kigwangalla akisema
“utaratibu uliovunjwa kwa mujibu wa kanuni ya 63 ni kusema uongo
bungeni, imethibitika bila shaka yoyote kwamba Mh James Mbatia
alilidanganya bunge, alilidanganya bunge na kusema atakua tayari
kujiuzulu mitaala hiyo ikiletwa”
Mh Kigwangalla alimalizia kwa
kusema “naomba atumie uungwana yeye mwenyewe kusimama katika bunge
hili.. aidha kuwaomba radhi Watanzania kwa kudanganya ama kutimiza
wajibu aliousema wa kujiuzulu, uongo aliousema ni mkubwa sana.. naomba
nitoe hoja kwamba Mh Mbatia aadhibiwe kwa mujibu wa kanuni ya 63,
asihudhurie vikao visivyozidi 20 na aombe radhi kwa maandishi kwa
Watanzania kwa kusema uongo bungeni”
Baada ya Mh Kigwangalla
kumaliza kuongea Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machari alisimama na
kusema “Mh Mbatia hakuzungumza uongo kutokana na ushahidi ambao hata
mimi ninao, waziri alilitaarifu bunge hili kwamba mitaala ya sasa
inayotumika ndani ya nchi yetu ni ya mwaka 2005 na kwa mujibu wa rasimu
ya mtaala tuliyonayo sisi inaonyesha iko mitaala miwili ambayo
imeandaliwa mwaka 2005 chapa ya kwanza mwaka 2012 jambo ambalo
linajustify kwamba baada ya kuulizwa mwaka jana ndio walianza kwenda
kutengeneza”
Mh Moses kwenye sentensi
nyingine namkariri akisema “ilikua ni swala la kwenda kuchakachua,
kupika na hicho kilichowasilishwa ndani ya bunge lako Mh Mwenyekiti
hatukua na imani toka mwanzo kwa sababu tunao waraka wa serikali, hatuna
imani na hata alichokua anazungumza Mh Kigwangalla kwamba Mh Mbatia
amedanganya, kwanza waanze waende wakaadhibiane wao wenyewe”
Kwa kumalizia namkariri
mwenyekiti wa bunge Jestina Mhagama akisema “hatuna kifungu ambacho
kinawaambia wabunge huyo mbunge sasa ajiuzulu ila mbunge mwenyewe
anapotoa kauli ya kujiuzulu, yeye mwenyewe anao uwezo wa kupima je kwa
haya yanayojiri yanafanya aendane na kile alichokisema, kwa yaliyotokea
nijiuzulu au nisijiuzulu… kwa hiyo iko mikononi mwa mbunge mwenyewe
lakini sisi kama Bunge hatuna mamlaka kwa mujibu wa kanuni kumwajibisha
huyo mbunge ajiuzulu”