PREZZO NA GOLDIE WANAFUNGA NDOA!!..
Posted on
Feb 9, 2013
|
No Comments
Najua kama umekua karibu na
internet wiki hii, stori kwamba Mastaa CMB Prezzo wa Kenya na Goldie wa
Nigeria wanafunga ndoa kuna uwezekano ukawa uliiona.
Ni stori ambayo kiukweli kwa
asilimia kubwa wameiamini manake haijaripotiwa kama fununu bali ni
taarifa kamili kupitia mitandao mbalimbali.
Ukweli ni kwamba sio taarifa za kweli, nimezungumza na Prezzo mwenyewe ambae namkariri akisema “sio kweli bro, ni uzushi tu”
Inaaminika Prezzo na Goldie
wako kwenye mapenzi mazito yaliyoanzia kwenye jumba la Big Brother 2012,
mapenzi ambayo hata hatua zao nje ya BBA ndio zimethibitisha kwamba bado wako pamoja mfano safari ya Marekani, Prezzo kwenda Nigeria na mengine.