MAKAM WA RAIS Dk. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF LEO.
Posted on
Mar 7, 2013
|
No Comments
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefungua Mkutano wa pili wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) jijini Dar es Salaam na kuzindua uuzwaji wa Nyumba za mradi wa
Mfuko huo pamoja na Uchangiaji wa hiyari kwa Watu wasio watumishi wa Umma.
Pichani
Meza kuu kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Fedha, Dk. William
Mgimwa, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Katibu Mwenyekiti wa
Bodi ya udhamini PSPF, George Yambesi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,
Adam Mayingu.
Makamu
wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi kitambulisho chake
Mwalimu Winfrey Ibrahim Banda baada ya kujiunga na mfuko huo kupitia
uchangiaji wa hiyari wakati wa Uzinduzi wake.
Sehemu ya
wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakifuatilia
mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Mkutano huo jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kushoto) akisalimiana na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Jaji Frederick Werema wakati viongozi hao wawili
walipokutana katika Mkutano Mkuu wa wadau wa PSPF jijini Dar es Salaam
leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF,
Adam Mayingu.