KENYATTA ATANGAZA MAJINA 12 YA MAWAZIRI
Posted on
Apr 25, 2013
|
No Comments
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akishirikiana na Makamu wa Rais William Ruto leo ametangaza kwa mara ya pili majina 12 ya Mawaziri watakaounda Baraza jipya.
Orodha ya leo imefanya idadi ya Mawaziri hao walioteuliwa kufikia Mawaziri 16 huku wananchi wakiendelea kusubiri nafasi mbili kwani awali Rais Kenyatta aliutangazi umma kuwa baraza lake la mawaziri litakuwa na watu 18 tu.
Miongoni mwa mawaziri walioteuliwa leo na wizara zao zikiwa kwenye mabano ni Najib Balala( Madini ), Charity Ngilu (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya mijini ), Adan Mohamed ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Baclays Afrika (Viwanda na Maendeleo ya Biashara).
Wengine ni Anne Waiguru(Maendeleo ya wananchi na Mipango), Felix Tarus Kosgey(Kilimo, Mifugo na Uvuvi), Judy Wahungu(Maji na Maliasili), Hassan Wario(Michezo na Utamaduni), Jacob Kaimenyi (Elimu) Francis Kimemia (Katibu wa Baraza la Mawaziri) na Lawrence Lenayapa (Mnadhimu wa Ikulu).
Kwa habari zaidi ungana nasi baadaye