photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > BI KATE AJIFUNGUA MTOTO MVULANA.

BI KATE AJIFUNGUA MTOTO MVULANA.

Posted on Jul 23, 2013 | No Comments




Mkewe mwanamfalme wa Uingereza Kate Middleton amejifungua mtoto wa kiume..ndilo lilikuwa tangazo kutoka Kasri la Kensington . Tangazo rasmi liliwekwa nje ya kasri hilo kwa watu kujionea.




Katibu wa mawasiliano wa Ufalme Ed Perkins alitoka kwa haraka nje ya hospitali kuwasilisha taarifa ya kuzaliwa kwa mtoto



Maelfu ya watu walisubiri nje ya hospitali alikozalia Bi Kate , walikuwa wanasubiri tangazo rasmi la kuzaliwa kwa mtoto



Tangazo hilo pia lilikuwa habari zilizopeperushwa duniani kote na hapa katika medani ya Times Sqaure mjini New York Marekani





Marcus Setchell (katikati) aliyeongoza madaktari waliomzalisha Bi Kate aliondoka nje ya hospitali kusema kuwa ''Mtoto mzuri na mrembo amezaliwa



Medani ya Trafalgar itakuwa na mwangaza huu kwa wiki nzima kusherehekea kuzaliwa kwa mwanamfalme




Bi Kate alipelekwa hospitalini mapema jana akiwa anaumwa uchungu wa uzazi. Alisafiri kwa gari akiwa na mumewe Prince William wa Cambridge.





Mamia ya watu wakiwemo waandishi wa habari walikusanyika nje ya hospitali alikozaliwa mwanamfalme ya St Mary's mtaa wa Padington , mjini London.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru