photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MELI YA MV KARAMA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR.

MELI YA MV KARAMA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR.

Posted on Jul 18, 2012 | No Comments




Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia kwa mashuhuda Meli hiyo MV Karama ya  Kapuni ya Seagal imezama baada ya kupinduka kichwa chini miguu juu katika eneo la Chumbe karibia na Visiwa vya Zanzibar.

Mashuhuda hao wanakisia kuwa takribani watu 200 walikuwa ndani ya meli hiyo hata hivyo watu kadhaa wameonekana wakiwa wanelea huku wakiwa wamevaa (Life Jackets) na kuwa boti zisizopungua 4 zimeshafika eneo la tukio kwa ajili ya kuwaokoa na Wahanga wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

 Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru