photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM AMBASSADOR KHAMIS KAGASHEKI AT THE SEATTLE SOUNDERS FC IN USA

MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM AMBASSADOR KHAMIS KAGASHEKI AT THE SEATTLE SOUNDERS FC IN USA

Posted on Jul 18, 2012 | No Comments

  Ministry Kagasheki, Dk Aloyce Nzuki and  Mussa Ibahim  walk across the pitch at Century Link Field in Seattle, Washington with the massive Tanzania advertising in the background

Timu ya Seattle Sounders FC imetangaza ushirikiano na Tanzania, nchi ambayo ni nchi kubwa kabisa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Ushirikiano huo ulitiwa saini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki (Mbunge) na Mmiliki wa timu ya Seattle Sounders Joe Roth katika hafla fupi iliyofanyika jana mjini Renton.

Mbali ya Waziri Kagasheki, wengine walioshuhudia kutiwa saini kwa ushirikiano huo ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki  na maofisa wengine kutoka Wizara ya Utalii, Ubalozini na maofisa wa Seattle Sounders FC. Mambo muhimu katika ushirikiano huo ni uwekwaji wa alama za vivutio vya utalii vya Tanzania katika maeneo mbali mbali kama CenturyLink Field na Starfire Sports Complex,  uwanja wa mazoezi wa Sounders FC uliopo eneo la Tukwila.
 Vivutio mbali mbali vya Utalii wa Tanzania vitawekwa katika maeneo hayo kama picha za Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na Zanzibar.
"Ushirikiano wetu na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) utasaidia kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania nje ya mipaka yake kwani kuna vivutio vya ajabu mno na kuleta unafuu kwa watalii ,” alisema Mmiliki wa timu ya Sounders FC,  Joe Roth. Na kuongeza kuwa ushirikiano huo utatoa nafasi muhimu kwa  soko la Utalii wa Tanzania nchi ya mipaka yake.
 Waziri Kagasheki mbali ya kupongeza kwa kufanikisha hatua hiyo muhimu katika sekta ya Utalii nchini alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa nyingi kwa Watanzania na Wamerekani kwani utahimarisha juhudi za Wizara ya Utalii katika kukuza soko la Utalii wa Kimataifa na wa Ndani.
Mheshimiwa Kagasheki pia alisema kuwa ushirikiano huo utatoa fursa za kibiashara kwa nchi zote mbili na kuongeza uwekezaji.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru