YANGA YAPIGWA 2-0 NA TIMU YA ATLETICO KAGAME CUP UWANJA WA TAIFA
Posted on
Jul 14, 2012
|
No Comments
Mchezaji wa timu ya Yanga Juma Abdul akijaribu kunyang'anya mpira kutoka kwa beki wa timu ya Atletico Henry Mbazumutima kwenye mchezo wa pili wa fungua dimba katika michuano ya kombe la Kagame inayoandaliwa na shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA inayofanyika jijini Dar es salaam Tanzania, Mpira umekiwasha na timu ya Yanga imeambulia kipigo cha magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezji Didier Kavumbagu wa Atletico
Wachezaji wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa wamefurika uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mchezo kati ya timu yao na timu ya Atleticokutoka Burundi.